Sunday, 17 April 2016

jiunge na group letu la whatsapp

jiunge na group la whatsapp uliza maswali kutana na wanafunz na walimu ndani ya group
wahi kabla nafasi hazijaisha
jiunge hapa bure
YOUR NAME :
YOUR EMAIL:
YOUR WHATSAPP NUMBER:

haki zote zimehifadhiwa +255-656-848274

Wednesday, 6 April 2016

jiunge na group letu la whatsapp

jiunge na group la whatsapp uliza maswali kutana na wanafunz na walimu ndani ya group
wahi kabla nafasi hazijaisha
jiunge hapa bure
YOUR NAME :
YOUR EMAIL:
YOUR WHATSAPP NUMBER:

Friday, 1 April 2016

Watu wengi huingia madukani kila mara kununua computer. Huweza kuwa Desktop au laptop kulingana na mahitaji yako. Kuna baadhi ya watu huniuliza swali hili, ninataka kununua laptop, unanishauri nichukue laptop gani?

 Unapohitaji kununua computer hasa laptop, kwanza kuwa makini na nini ungependa kufanya kwa kutumia laptop hiyo. Kama wewe ni mtaalamu wa masuala ya computer kwa shughuli nzito kama kudesign picha, video, beats lazima unahitaji computer yenye RAM kubwa(angalau 3GB) , video card kubwa, yenye hard disk(angalau 350GB) kubwa pia. Kwa matumizi ya nyumbani tu sio lazima iwe na RAM kubwa (2GB inatosha) au processor(1.5GHz inatosha) bali hard disk inabidi iwe na uwezo wa kutosha (Angalau 250GB).

Ewaa! Basi tusifanye mambo yawe marefu. Leo nitakutajia laptop 10, bora zaidi sokoni kwa sasa. Takwimu hizi zimekusanywa na watumiaji wengi wa computer duniani. Gharama na ubora wa laptop huenda sambamba. Lakini kumbuka kuwa kampuni iliyotengeneza laptop fulani sio lazima tu kila laptop yao inakidhi matakwa yako, zingatia Hard disk size, RAM, processor, video na graphics card, ukubwa na uzito pia ubora wa betri.

1. NANI ZAIDI YA APPLE!?

Niamini hakuna zaidi. Laptop za Apple, Macbook Air ndizo bora zaidi sokoni. Laptop hizi hutengenezwa kwa aluminium.Hutumia SSD ambazo zina kasi kama mara 4 zaidi ya Hard disk za kawaida. Zaidi Operating system yake ni safi na ya kipekee isiyoshambuliwa na virusi. Sababu kubwa ambayo huwafanya watu wasiwe na laptop hizi hasa hapa Afrika mashariki ni bei zake ghali.

2. Hewlett-Packard (HP)

Ubora: 4.5/5
Watumiaji:1/5

Huweza kukaa kwa muda mrefu. Ni ngumu, ni bora, ni bei NZURI. HP ni kampuni kongwe zaidi kupita Dell na wengine. Laptop zao ndizo zinazoaminika zaidi, ni bora zaidi na bado bei zake ni nzuri zaidi. Hii ndiyo laptop bora inayotumia platform kama Windows.

3. Dell. 

Ubora: 4/5
Watumiaji: 3/5

Zina warranty ya muda mrefu kupita computer zote sokoni. Dell huwa na speaker zinazotoa mziki mzuri. Pia uwezo wa screen zake ni mzuri sana. Ni bora kwa matumizi ya nyumbani na ofisini. Zina nguvu kubwa sana. Computer mpya za Dell Alienware ndizo laptop zenye nguvu zaidi kupita computer zote kwa sasa.

4. Asus.

Ubora: 4/5
Watumiaji: 0.5/5

Motherboard au ramani ni muhimu kwa kifaa chochote cha elektroniki. Asus ni kampuni inayokubalika kwa kutengeneza motherboard ambazo pia hutumiwa na makampuni mengine kama Dell, Acer na Lenovo. Hivyo basi lazima wao weyewe computer zao ziwe bora kwa akili ya kawaida tu. Asus hutengeneza laptop bora. Hupata Errors chache zaidi kama unatumia platform za windows na Ubuntu.

5. Acer

Ubora: 4/5      Watumiaji: 3/5

Kama unazungumzia laptop za kisasa hautaiacha acer. Kweli laptop hii ni bora  na ingestahili kuwa juu kabisa katika list hii kama isingekuwa ghali kidogo. Ina nguvu kubwa ya kufanya kazi na graphics pamoja na video. Acer zilizo na touch screen zinasemekana kuwa nzuri zaidi ya laptop nyingine zenye touch screen. Betri za acer pia ni bora kwa mujibu wa maoni mbalimbali ya watumiaji wake.
Listi ya 5 zilizobaki ni kama hii hapa chini.
6. Lenovo
7. Toshiba
8. Samsung
Ni ngumu kuamini kama kweli hii ndiyo nafasi ya samsung katika kumi hizi bora zaidi. Samsung ni moja kati makampuni bora zaidi ya elektroniki duniani. Hutengeneza bidhaa nyingi na bora. Uwezekano wa idadi kubwa ya watu kutumia laptop zao uko chini kupita jinsi watu wanavyoamini simu zao. Laptop za samsung zimekuwa zikipata hitilafu mara nyingi zaidi ya hizo nyingine. Hata hivyo laptop hizi ni poa zaidi, si unajua tena, made in Seoul, China.

9. Alienware
10.Sony.

Shukrani kwa kuendelea kuwa mgeni wa Suparoja studio. Tafadhali kama kuna swali lolote lihusulo computer na teknolojia kwa ujumla usisite kuniachia swali hilo katika kipengele hapo chini ya screen kilichoandikwa NIKUFANYIE NINI? na nitakupatia majibu na ufumbuzi. Ni faraja kwangu kuweza kukusaidia pia unaweza kunipigia simu kwa namba inayopatikana katika kipengele cha about. #Asante_kwa_kuwepo.

HOW TO CHANGE INTERNAL HARD DISK TO BECOME EXTERNAL

Freeze your hard drive to recover data: Recovering data from a clicking hard drive can be a touch and go task. In most cases, a clicking hard drive signifies that the drive is stuck in seek mode and is a sign that your drive is failing. In most cases, if the clicking hard drive contains the operating system you boot from, you will lose the ability to boot from this device (it will just sit there clicking away) and the drive will appear to be dead. In which case, many people assume the drive is shot and data cannot be retrieved.

However, what most people don't know is that properly freezing a clicking (failing) drive can enable you to quickly backup the important data. Here is how the process works:

How to backup data from a clicking hard drive:

1. First, remove the clicking hard drive from your computer and place it in a ziplock bag (to prevent condensation)
ziplocked-drive.jpg

2. Place the zip-locked hard drive in the freezer for an hour
hard-drive-freezer.jpg

3. Have a backup storage device handy such as an external USB hard drive or large flashdrive
4. Remove the hard drive from the freezer and immediately reconnect it to your computer. Important: The drive does not need to be mounted in the carriage, however, make sure the hard drive is resting on a flat surface. The picture below does not portray this.
connected-drive.jpg

5. Attempt to boot your computer again. In most cases, the drive will boot right up. In other cases it may take a few attempts.
6. Once booted, connect your backup device and attempt to "copy" the information you wish to retrieve over to the USB backup storage device

Note: You will only have a 15-20 minute window within which to completely backup your data. This is the typical thaw time, which may vary depending on environmental heat factors.
U

Hivi karibuni mdau mmoja wa blog hii alinitumia e-mail na kuniuliza ni kwa jinsi gani anaweza kuipata simu yake iliyopotea, hasa kwa kutumia mtandao. Juhudi zangu za kutambua ni aina gani ya simu aliyoipoteza mdau huyu bado hazijazaa matunda lakini ni matumaini yangu kuwa ataweza kusoma post hii maalumu kwa ajili yake na wote wenye tatizo kama lake.

Hivi sasa tunapoongelea simu, tunaegemea sana kwenye smartphone. Smartphone kwa kiasi kikubwa ni nyepesi kufanya shughuli nyingi ikiwemo shughuli za usalama. Hivyo kwa kutumia uwezo wake huo tutaona jinsi ya kuipata pindi inapopotea au inapoibwa. Lakini pia kama unatumia simu ya kiganjani ya kawaida tutatizama pia jinsi ya kuipata.

Kama simu yako iliyopotea ni ya Apple ningependa ubofye hapa uendelee na Apple moja kwa moja.

Jinsi ya kupata simu iliyopotea: Android:

Simu hizo huwa moja wapo kati ya hizi: TECNO,  SAMSUNG  SONY,  na nyingine nyingi za aina hizi.

Kama simu yako iliyopotea ni android usiwe na wasiwasi. Hebu tufuatilie njia zifuatazo zinazoelezea kwa kina namna gani ya kuweza kuipata simu yako.

>>  Kwa kutumia ANDROID DEVICE MANAGER (ADM).

Je, unatumia Google Play Store. Jibu lako bila shaka ni ndio na kama sio basi hakikisha umejiunga na Play Store. Kwa nini nimeanza na hili ni kwa sababu ili kujiunga na Play Store lazima uwe na akaunti ya Gmail. Kwa nini Gmail, kwa sababu hii ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kutambua pahala simu yako ilipo. Android Device Manager ni programu ya google inayopatikana karibu katika kila smartphone ya android. Usijiulize maswali mengi na hata kama haujawahi kuiona usiwaze, hii hufanya kazi ndani ya smartphone yako. Jaribu kuisachi kama usipoipata unaweza kidownload kupitia Play Store au  bofya hapa.

Programu hii itatusaidiaje?
ADM hufanya kazi ya kutambua pahala simu yako ilipo kwa wakati husika endapo imeunganishwa na mtandao wa internet. ADM pia huweza kulock au kufuta simu nzima kama umeifanyia settings.  Kama simu yako imepotea au imeibiwa fanya yafuatayo ili kuipata.

  • Ni rahisi sana. Kama umetimiza yote hapo juu, punde tu unapogundua simu yako imepotea tafuta laptop/computer au simu ya android nyingine yoyote. Sign-in katika gmail kupitia kifaa hicho. Ukisha Sign-In tembelea tovuti ya ADM hapa. Au search tu google 'Android Device Manager' na chagua tovuti yao pale juu kabisa. 
  • Tovuti hiyo ikishafunguka utaweza kuchagua kifaa chako (Smartphone/Tablet) ambayo imeshajisajili kupitia e-mail yako ya gmail.

  • Baada ya kuchagua Google itakuonesha ramani ya wapi simu hiyo ilipo. Baada ya hapo unaweza kuchagua kitufe cha ring. Hata kama aliyeiiba ameshabadili line simu hiyo itaita kwa muda wa dakika kama tano.

  • Zaidi pia ni jinsi ya kulock simu yako kupitia huduma hii hii ya ADM. Utaweza kufanya hivyo kwa kuchagua kitufe cha Lock. Kumbuka kitufe hiki kifanya kazi endapo ulifanya settings za kuruhusu ADM kulock na kufuta simu. Faida moja wapo pia ya kutumia option hii ya Lock ni kwamba unaweza kuandika ujumbe ambao yeyote mwenye simu hiyo kwa wakati huo ataiona.

  • Pia unaweza kufuta data zote zilizopo katika simu yako hiyo kama unahisi imeibwa au imepotea kabisa kwa kubonyeza kitufe cha Erase. 

Njia hii huweza kufanya kazi endapo tu, umeshajiunga na gmail, na pia simu iwe imeunganishwa na internet. Hii ndiyo njia bora kwa mujibu wangu. Usipofanikiwa mara ya kwanza endelea kujaribu usikate tamaa, kama mwizi ameiba smartphone lazima nyakati fulani ataingia tu katika mtandao. Akiingia tu basi kajichanganya. Ni vyema utoe taarifa polisi ni wajibu wao kuhakikisha usalama wako na mali zako.

Kwa kutumia PLAN B
Plan B ni app ambayo imetengenezwa kama suluhisho wa ADM. Plan B inakuwezesha kutambua mahali simu yako ilipo kwa kuinstall programu kupitia mtandao. Hii inakusaidia kama mwanzo haukuwa na ADM na kwa sababu imepotea hauna uwezo wa kudownload na kuinstall. Plan B itakutumia SMS kila baada ya dakika 10 kukupa taarifa juu ya simu yako na mahali ilipo.

Njia nyingine  ni pamoja na kutumia apps ambazo itabidi uzi install kabla ya kuibiwa (:))
Apps hizo ni kama hizi zifuatazo:
Unaweza kutumia Google Maps pia kufuatilia mwenendo wa simu yako. Kama una akaunti ya Gmail utakuwa tayari umeunganishwa na Google Maps. Tembelea Google Maps kisha nenda katika Settings chagua Location History. Kwa njia hii utaweza kugundua mahali simu yako ilipo.

Je kama simu yangu sio smart kivile?

Kama simu yako ni simu tu ya kawaida ya mawasiliano kama Nokia ya tochi, inapoibiwa au kupotea siyo rahisi kuitafuta kwa njia ya mtandao. Kama unaifahamu IMEI namba, ambayo ni tofauti kwa kila simu unaweza kuiunganisha simu yako hapa katika mtandao wa TrackImei na itaweza kutafuta mahala simu hiyo ilipo pindi itakapo potea.

Asante kwa kusoma hii. Shukrani kwa kuwa nasi mwaka mzima wa 2014. Mipango yetu kwa ajili yako ni mikubwa zaidi 2015. Endelea kuwa nasi.

Youtube ni tovuti maarufu sana duniani inayojihusisha na masuala ya kushare videos, ni mahali ambapo unaweza kupata si tu videos za muziki na burudani bali pamoja na videos za kuelimisha na kujifunza masuala mbalimbali. Mara nyingi watumiaji wa Youtube hupenda kupakua (download) videos  zinazowavutia kwa matumizi ya baadaye, lakini Youtube haina uwezo (feature) hii "by default".

Kwa watumiaji wa kompyuta mambo huwa ni rahisi kidogo linapokuja suala la kupakua videos kutoka Youtube. Wengine huweka programu maalum kwa kufanya kazi hiyo, programu kama Internet Download Manager (IDM) kutoka Tonec Inc au Free Youtube Downloader,AllMyTube , Free Video Converter na Video Converter Pro zote kutoka Wondershare hufanya suala la kupakua videos kutoka Youtube kuwa rahisi sana. 

Pia kwa wale wanaotumia browser kama Chrome pamoja na variants zake wanaweza kuwekaextensions zenye kufanya kazi hiyo (Youtube/Video Downloaders) ambazo zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome inayojulikana kama Chrome WebStore. Lakini pia ili kufanikisha mchakato wa kupakua videos hasa zilizopo Youtube kuwa rahisi zaidi unaweza kutumia browsers kama Baidu Browser au Spark Security Browser ambazo zimetengenezwa
zikiwa na uwezo wa ndani (built-in capability) wa kupakua video kutoka katika tovuti kama Youtube, hauhitaji extension wala programu yoyote kuwezesha hilo, browser husika ndiyo ina uwezo huo.

Kwa wale wanaotumia smartphone (Android) kutembelea Youtube, si rahisi kupakua video hizo! si tu kwa kutumia browser ya simu, bali hata kwa app rasmi ya Youtube inayopatikana Google PlayStore. Lakini kwa kutumia app inayoitwa OGYoutube suala hili si gumu tena.  OGYoutube ni modded app(modding ni muongezo au boresho la software ili iweze kufanya kazi zaidi ya vile inavyopaswa) inayokuwezesha kupakua video kutoka Youtube moja moja katika smartphone yako. Kifupi ni app ya Youtube iliyoongezewa uwezo (features).

Features za OGYoutube
1. Pakua (Download)  video zaidi ya moja kwa muda mmoja.
2. Angalia na download video katika ubora (video quality) wowote unayotaka, kuanzia 144p hadi 1440p

Download
Ubora wa Video

3. Pakua Subtitle za video husika.

4. Popup Player, angalia video huku ukiwa unaendelea kutumia simu kwa kufanya mambo mengine.

Subtitle
Popup Player

5. Pakua video ikiwa katika mfumo wa sauti tu (MP3).

6. Pia unaweza angalia video hata screen yako ikiwa katika lock.

Downloads

Link:  Download OGYoutube   HAPA  OGYoutube v0.9
Official Webiste:   OGMods

Kumbuka

1. Ili kuinstall app hii, lazima uwe umeruhusu simu yako kuweza kuinstall apps kutoka katika vyanzo visivyo rasmi (unknown sources)
Kama bado, Ingia katika "Settings" ya simu yako, kisha nenda katika "Security". Ndani ya security tafuta mahala palipoandikwa "unknown sources", hakikisha sehemu hii ipoactivated.

2. Baada ya kuinstall itatengeneza shortcuts mbili, ya kwanza ndiyo app yenyewe (OGYoutube), na ya pili ni shortcut yenye jina la Downloads,  ambayo itahifadhi videos unazopakua kutoka Youtube.

Je, imekusaidia? Hakikisha inamsaidia na rafiki yako pia,  Share!!  & Comment!!

Popular Posts